Lengo letu

Kuwasaidia na kuwafundisha viongozi kanisani vijana mpaka wazee katika Afrika mashariki. Tunapenda kuwaongoza wanafunzi katika imani ndani ya Kristo na kuwatayarisha kwa huduma.

Sisi ni nani?

Tawi la AIC Diguna

Diguna Discipleship Training (DDT) ni tawi la umisheni wa AIC (Africa Inland Church) Diguna. Katika Diguna Waafrika na wazungu wanafanya kazi pamoja kusudi kueneza Injili ya Bwana Yesu Kristo.

Ukipenda kujua zaidi kuhusu DIGUNA upige hapa

Kutayarisha kwa huduma

Tuna hamu kuwafunza wanafunzi katika imani ndani ya Yesu na kuwafundisha kufanya huduma.

Kujifunza na kufanya

Hatutaki kuwafundisha wanafunzi kielimu tu bali waweze kutia mafundisha katika maisha yao binafsi na huduma. Kwa mfano katika kosi za Kiingereza wanafunzi watafundishwa kutumia Computer vizuri.

Kiswahili na Kiingereza

Tunazo kosi mbalimbali katika mwaka. Kosi za Kiswahili ni kwa watu wanaokaa katika huduma kanisani au wanaotaka kujitayarisha kwa huduma kama wachungaji bila chuo cha Biblia, wazee wa kanisa, wainjilisti, viongozi wa vikundi, walimu wa shule ya Jumapili na kadhalika.
Kosi za Kiingerezi zinalenga vijana waliomaliza shule (hasa kidato cha nne) kuwasaidia katika maisha yao kumfuata Yesu na kupanga maisha yao pamoja na Yesu ili wapate kuwa watu waaminifu katika nchi.

Walimu wetu

Hans Seppi

Hans na mkewe Jacqueline wametoka Switzerland na walibarikiwa na watoto watano. Wameishi nchini Kenya kwa miaka mingi. Hans anajulikana vyema kwa kuanzisha shule ya DIGUNA Discipleship Training miaka thelathini iliyopita. Hans ana ujuzi mwingi katika kufundisha na kuelewa nchi ya Kenya na watu wake pia. Anazungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha. Na huo ujuzi Hans alianza kusaidia katika kuanzisha kanisa jipya la A.I.C. katika eneo la Rongai. Anapenda kufundisha katika DDT. Yeye huyafanya mafundisho yake kuwa rahisi na ya kueleweka.

Fred Olima

Fredrick Olima alikua mwanafunzi wa DDT mwaka 2012, katika kosi ya Young Leaders Training. Baadaye alijiunga na chuo cha Bibilia, Moffat Bible College, pahali ambapo alisomea Thiolojia na Ushauri wa Kikristo. Alikuwa mchungaji wa kujitolea katika A.I.C Bondo Town kwa muda wa miezi minne kabla ya hajajiunga na DDT mwaka wa 2017 kuwa mwalimu. Akiwa chuo cha Biblia, alifanya kazi na Cure International Hospital kwa miaka mitatu kwa kujitolea, na alisaidia katika Shule ya pili mbalimbali. Pia alisaidia na Nairobi Children Remand Home (approved school) kuwa mshauri. Kwa sasa amejitolea kusaidia kanisa la A.I.C Rangau. Furaha yake ni kuwaleta wanarika kwa Yesu. Hajaoa.

Fred Olima
John Kinyanjui

John Kinyanjui

Mimi ni Mchungaji John Kinyanjui na nimehudumu na Kanisa la Africa Inland katika Uasin-Gishu, Laikipia na Nyandarua hadi mwanzo wa 2018 nilipojiunga na Shule ya Diguna Disccipleship Training. Hapo ninawafundisha na kuwatayarisha wanafunzi kwa kazi ya huduma ili sote tuufikie umoja wa imani na kumfahamu sana mwana wa Mungu hata kufikilia kimo cha utimilifu wa Kristo.