Discipleship Training

Jambo kuu ni kuwaleta watu kwa Yesu! Utajifunza hapa maana ya wokovu na pia jinsi ya kumsaidia mwingine kufahamu wokovu njia ya kuongea mtu kwa mtu na katika kuhubiri.

Yaliyomo

Lengo kuu katika kosi hiyo ni ‘kuwaleta watu kwa Yesu’! Utajifunza hapa maana ya wokovu na pia jinsi ya kumsaidia mwingine kufahamu wokovu njia ya kuongea mtu kwa mtu na katika kuhubiri.
Ukiwa mwinjilisti, mzee wa kanisa au kiongozi wa kikundi kanisani kosi hii ni muhimu kwako.

Kwa jumla:
Karo inagharamia masomo, kukaa, chakula na vifaa vingine.
Pesa za kujiandikisha ni sehemu ya karo.
Mtu akikosa kujiandikisha vizuri anaweza kukosa nafasi.
Baada ya kila kosi mwanafunzi atapata cheti cha Discipleship Training.

Jambo kuu la kosi:
Kuwaleta watu kwa Yesu.

Masharti ya kujiunga:

  • Umeokoka
  • Una ushuhuda mzuri kanisani na nje.
  • Umri wako ni miaka 19 au Zaidi.
  • Unaweza kusoma na kuandika Kiswahili.
  • Unafanya huduma kanisani au unajitayarisha kufanya.
  • Ujiandikishe kirasmi na pesa za kujiandikisha (KSH 500)
Image

Tarehe

9th Sept. – 16th Nov. 2024 (wiki 10)

Image

Karo

KSH. 10,000

Image

Lugha

Kiswahili

Yaliyomo

  • Ushirika pamoja na Mungu.
  • Uhusiano kati ya wanamume na wanawake.
  • Wokovu
  • Jinsi ya kuwaleta watu kwa Yesu.
  • Roho Mtakatifu
  • Madhehebu mabaya (cults).
  • Kuwashuhudia Waislamu.
  • Umisheni
  • Wafilipi
  • Waamuzi
  • Kuhubiri
  • Wiki 2 za uinjilisti.
  • Kufunza Shule ya Jumapili.
  • Na mambo mengine.

Cheti cha Huduma ya Kikristo

Wanafunzi watapata Cheti cha HUDUMA YA KIKRISTO baada ya kumaliza Discipleship Training (wiki 10), Biblia na Huduma (wiki 10), Kazi ya nyumbani.
Wanafunzi wanaweza kumaliza sehemu zote 3 kwa wakati wao wenyewe

Placeholder

Sehemu ya 1 - Discipleship Training

wiki 10


Placeholder

Sehemu ya 2 - Biblia na Huduma

Kuijua Biblia (wiki 4), Huduma kanisani (wiki 4), Umisheni (Kampeni) (wiki 2)

Placeholder

Sehemu ya 3 - Kazi ya nyumbani

Discipleship Training