Kosi kwa walimu wa shule ya Jumapili
Wewe ni mwalimu wa shule ya Jumapili au unapenda kuwafundisha watoto. Katika kosi hii utapata mawaida jinsi ya kuwafundisha watoto ili wafahamu Biblia na imani katika Kristo
Yaliyomo
Wewe ni mwalimu wa shule ya Jumapili? Kazi hiyo ni muhimu sana kujenga mtu, jamii, kanisa hata taifa. Tunapenda kukusaidia kufanya kazi hiyo vizuri zaidi. Katika kosi utajifunzi jinsi ya kuwafikia watoto kulingana na rika zao. Pia utapata kitabu kinachokusaidia kuwafundisha watoto mwaka mmoja mzima.
Yaliyomo ya kosi:
Tunatumia kitabu cha CLMC (Christian Learning Material Centre)
Kwa jumla:
Karo inagharamia masomo, kukaa, chakula na vifaa vingine.
Pesa za kujiandikisha ni sehemu ya karo.
Mtu akikosa kujiandikisha vizuri anaweza kukosa nafasi.
Baada ya kosi mwanafunzi atapata cheti cha Discipleship Training.
Masharti ya kujiunga:
Tarehe
5th Oct. – 11th Oct. 2025 (wiki 1)
Karo
KSH. 3,000
Lugha
Kiswahili
Yaliyomo
Cheti cha Huduma ya Kikristo
Wanafunzi watapata Cheti cha HUDUMA YA KIKRISTO baada ya kumaliza Discipleship Training (wiki 10), Biblia na Huduma (wiki 10), Kazi ya nyumbani.
Wanafunzi wanaweza kumaliza sehemu zote 3 kwa wakati wao wenyewe
Sehemu ya 1 - Discipleship Training
wiki 10
Sehemu ya 2 - Biblia na Huduma
Kuijua Biblia (wiki 4), Huduma kanisani (wiki 4), Umisheni (Kampeni) (wiki 2)