11.jpg
Diguna Discipleship Training PDF Printi Imeili

Ni chuo rasmi cha Africa Inland Church, Kenya.

Diguna Discipleship Training ilianzishwa mwaka 1986 Lengo la chuo:Katika Africa mashariki hasa katika nchi kama Kenya, Tanzania, Uganda kila mwaka yameanzishwa makanisa mapya mengi. Makanisa haya ni madogo na washiriki hawawezi kumwajiri mchungaji. Kwa sababu hii mchungaji mmoja anahitaji kusimamia makanisa mengi. Matokeo ni:

  • Mchungaji hawezi kulitunza kanisa vizuri wala kuwapa washiriki msaada ule wanaohitaji.
  • Wazee lazima waongoze kanisa kama mchungaji.
  • Kwa sababu mara nyingi wazee hawakupata msaada na mafundisho ya kufanya kazi hiyo, hali ya kiroho ya kanisa inabaki chini sana.
  • Mara nyingi vijana hawapati msaada kwa maisha yao, wanaenda kuhudhuria kanisa lingine.

Tunaamini wazee na wote wanaofanya huduma fulani katika kanisa ni watu muhimu zaidi lakini wanahitaji msaada yaani mafundisho. Kwa sababu hii Diguna Discipleship Training ilianzishwa kuwasaidia wafanya kazi wa kanisa kama wazee, wainjilisti, walimu wa shule ya Jumapili, viongozi wa youth, viongozi wa akina mama, ….

Kila mtu anaweza kujichagulia kosi ambazo anahitaji kwa huduma yake. Hiyo kosi itamsaidia kufanya huduma yake vizuri zaidi kwa sababu kama kila kosi inalenga huduma.

Cheti:
Baada ya kumaliza kosi mwanafunzi atapata cheti cha kuhudhuria.
Kuna vyeti vinne maalum kwa wale wanaohudhuria kosi mbalimbali au 3 years Certificate Program.

Nani anaweza kujiunga na kosi?

  • Mwanaume na mwanamke aliyeokoka.
  • Anayefanya huduma fulani kanisani au anayetaka kujitayarisha kwa huduma fulani.
  • Mtu aliye na ushuhuda mzuri kanisani na nje ya kanisa.
  • Awe na miaka 19 au zaidi.
  • Ajue kusoma na kuandika Kiswahili.
  • Kwa kosi maalum lazima apite kwanza kosi nyingine
 

Bible Quiz

What is the last of the Ten Commandments?
 
(C) 2010 Delpy & Krayss. All rights reserved.